Mtihani wa Kuwekwa katika Darasa
Mtihani wa kuwekwa katika darasa sahihi kwa wanafunzi wa ESL
Mtihani wa kuwekwa katika darasa sahihi wa Kiingereza kama Lugha ya Pili (ESL, English as a Second Language) unahitaji kufanywa na wanafunzi ambao Kiingereza si lugha yao asili. Mtihani wa kuwekwa katika darasa sahihi wa ESL una sehemu 2. Hakuna kikomo cha muda wa kufanya mtihani huo. Kwa wanafunzi wengi, mtihani huo kwa kawaida huchukua kati ya saa 2 unusu hadi saa 3. Wanafunzi hawaruhusiwi kuwa na mkalimani wakati wa kufanya Mtihani wa Kuwekwa katika Darasa Sahihi wa ESL.
Sehemu ya 1: Mtihani wa ESL wa ACCUPLACER
Mtihani huu wa kompyuta una maswali 20 ya kuchagua majibu katika kila sehemu ifuatayo:
- Kusikiliza – kupima uwezo wako wa kusikiliza na kuelewa mtu mmoja au wengi wanaozungumza Kiingereza
- Kusoma – kupima uwezo wako wa kusoma Kiingereza kupitia ufahamu wa vifungu vifupi
- Matumizi ya lugha – kupima ustadi wako katika kutumia sarufi sahihi katika sentensi za Kiingereza
- Ujuzi wa sentensi – kupima uwezo wako wa kuelewa maana ya sentensi za Kiingereza
Sehemu ya 2: Sampuli ya uandishi
Utahitajika kuandika mwenyewe insha kuhusu mada utakayopewa. Kitengo cha ESL cha TCC kitahakiki insha yako ili kutathmini ujuzi wako wa kuandika.
Utapewa alama ya mtihani wa ACCUPLACER utakapoukamilisha. Ripoti yako ya kuwekwa katika darasa sahihi na mapendekezo ya kozi yatatumwa kwa anwani yako ya barua pepe ya TCC baada ya karibu siku 3 za kazi, baada ya kuhakikiwa kwa sampuli yako ya uandishi.
Baada ya kupokea vitu hivi, panga miadi ya kukutana na mshauri wa chuo ili ujiandikishe katika madarasa yanayofaa. Hakikisha umebeba ripoti yako ya kuwekwa katika darasa sahihi na mapendekezo ya kozi unapohudhuria miadi yako.
Sampuli ya Maswali ya Mtihani wa Kuwekwa katika Darasa Sahihi
Makala Yanayohusiana